Mahitaji gani maalum ya afya kwa wasichana
Wakati mwingine kati ya miaka 10 na 15, mwili wa msichana huanza kukua na kuanza kukomaa. Miaka hii yaweza kuwa ya kufurahisha na pia magumu. Msichana wa umri ya kati huwa hajui kama yeye ni mwanamke aliye komaa au mtoto. Mwili wake uko mahali katikati ambapo hajazoea. Hili jambo laweza kuwa ngumu msichana asipo pata mtu wa kumpa mawaidha kwa hiyo anaweza kosa kujua cha kutarajia.
Jambo muhimu kabisa ambalo msichana anaweza kufanya ni kula vizuri ili kuwa na afya njema. Mwili wake unahitaji kupata protini, vitamini na madini yanayohitajika katika miaka yake ya kukua. Msichana huhitaji chakula cha kutosha kama kile apatiwacho mvulana. Kupata chakula cha kutosha huzuilia magonjwa, husababisha kufanya vizuri shuleni, uja uzito wa afya, kuzaa salama na kuzeeka vyema.
Wasichana pia huhitaji chakula kinachowafaa. Wakati msichana anapoanza kupata damu yake ya mwezi hupoteza damu kila mwezi. Kuzuia upungufu wa damu atahitaji kula chakula ambacho kina virutubisho vya kutosha ili kuongeza damu mwilini mwake. Wanawake na wasichana huhitaji madini ya calcium kusaidia mifupa yao iwe na nguvu.