Malaria ni nini

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Malaria ni ugonjwa hatari unaosambazwa na mbu. Malaria hupatikana sehemu nyingi ulimwenguni. Katika Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, malaria inaongoza katika kusababisha vifo, magonjwa na ukuaji na maendeleo mabaya miongoni mwa watoto wachanga. Inakadiriwa kuwa mtoto mmoja hufa kila sekunde thelathini kutokana na malaria sehemu hii.

Malaria husambazwa wakati mtu anapoumwa na mbu aina ya anopheles. Mbu huyu huhamisha vimelea vya malaria, plasmodium, kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Watu hugonjeka sana na kuwa na joto kiwango cha juu, kuendesha, kutapika, kuumwa na kichwa, kuhisi baridi na kua na dalili kama za homa. miongoni mwa watoto sanasana, ugonjwa huu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa haraka na kusababisha ukosefu wa fahamu na kifo. Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa huu kwa sababu kinga yao bado ni hafifu sana kukabiliana na ugonjwa huu.

Sources