Mazoezi yapi yatakayo nisaidia kutuliza na kuongeza nguvu kwenye mgongo na viungo vyangu vya tumbo
Jaribu kufanya mazoezi haya kila siku, kwa mpangilio ilivyo orodheshwa:
1. Kunyoosha upande wako wa chini wa mgongo: Lala kwa mgongo wako kisha kumbatia magoti. Shikilia njia hiyo kwa sekunde 10-15 ukipumua kwa nguvu. Ukiwa unavuta pumzi nje, kwa utaratibu songeza magoti karibu zaidi na kifua chako ili kuongeza mnyooko. rudia mara 2, au hadi utakapo hisi uwachilio kwenye mgongo wako wa chini
2. Mgeuzo Lala kwa mgongo wako huku ukiwa umenyoosha mikono zako kwa upande. kunja magoti zako, kisha zisongeshe polepole kwa upande mmoja. Kwa wakati huo, geuza kichwa chako kwa upande mwingine, jaribu kuweka mabega yako chali kwenye sakafu. Baki kwenye nafasi hii huku ukivuta pumzi ndani na nje kwa mda zaidi. Sasa inua magoti yako katikati, kisha pole pole zilete kwa upande mwingine. Geuza kichwa chako upande mwingine. Rudia zoezi hili mara mbili kwa pande zote, au hadi utakapohisi uwachilio kwenye mgongo wako wa chini
3. Mkunjo wa sehemu ya chini ya Kiuno Lala kwa mgongo wako huku ukiwa umekunja magoti. Lalisha sehemu ya chini ya mgongo wako kwenye sakafu. Polepole shikanisha kwa nguvu sehemu yako ya chini pia misuli za nyonga kisha shikilia huku ukihesabu hadi tatu. Endelea kuvuta pumzi ukishikilia. Ukiendelea, mgongo wako utajikunja kwa juu kama kawaida inavyofanya. Rudia