Mbona kuvuta sigara ni hatari zaidi kwa mimi kama mwanamke - Audiopedia
Kuongezea hizo shida zingine zilizotajwa, wanawake wanaovuta sigara wana hatari kubwa ya:
- kupata shida kupata mimba (utasa)
- kuharibika kwa mimba, na watoto wanaozaliwa wadogo sana au mapema sana.
- kuwa na shida wakitumia dawa za kupanga uzazi.
- kukata hedhi mapema.
- kuwa na mifupa yanayovunjika kwa urahisi zaidi kuliko wengine uzeeni na hata kati ya maisha (osteoporosis).
- saratani ya mfuko wa uzazi au tumbo/uterasi.
Mwanamke mjamzito anafaa ajaribu kuepuka watu wanaovuta sigara ili moshi huo usidhuru mtoto yake.
Sources
- Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
- Audiopedia ID: sw010316