Mbona madini aina iodine ni muhimu kwa mtoto wangu
Viwango vidogo vya madini aina iodine ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto. . Ikiwa mwanamke hatapata madini haya wakati yeye ni mja mzito, huenda mtoto wake atazaliwa akiwa na shida za kiakili au, shida za kusikia na kuzungumza. Ikiwa mtoto hatapata madini haya wakati akiwa mchanga, basi atachelewa kukua kimwili, kiakili na utambuzi. Kukosa madini haya kunaweza kuathiri uwezo wa kujifunza.
Goitre, ni uvimbe usio wa kawaida wa tezi ya dudumio. Uvimbe huu hutokea shingoni na ni ishara ya ukosefu wa madini aina iodine katika lishe. Ukosefu wa iodine mwanzoni mwa uja uzito unaweza kusababisha kuharibika kwa mimba au kufa kwa mtoto ambaye hajazaliwa.
Utumizi wa chumvi iliyo na iodine badala ya chumvi ya kawaida huwapa akina mama waja wazito na watoto viwango wanavyohitaji vya iodine. Chumvi iliyo na iodine ni salama kwa familia nzima na ndio chumvi tu inayohitajika kwa mapishi. Ni muhimu familia kuhakikisha kuwa wananua chumvi iliyo na iodine - na ambayo ina matangazo yanayoonekana. Akina mama wanahimizwa kutumia chumvi yenye iodine kabla na baada ya kujifungua. NI muhimu kwa akina baba na akina mama kuhakikisha kuwa watoto wanatumia chumvi iliyo na iodine.