Mbona malaria ina hatari zaidi miongoni mwa wanawake wajawazito

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Wanawake wajawazito wana uwezekano mkubwa kuugua ugonjwa wa malaria kuliko wanawake wengine. Ugonjwa huu ni hatarizaidi wakati wa ujauzito, sanasana ikiwa ni ujauzito wa mara ya kwanza. Sababu ya kiwango hiki cha juu ni kuwa katika ujauzito kuna mabadiliko mengi yanayoendelea katika mwili wa mwanamke hivyo kusababisha kinga yake dhidi ya ugonjwa huu kupunguka. Malaria yaweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu, kuharibika kwa mimba, kujifungua mapema kuliko wakati unaofaa na kujifungua mtoto aliyekufa.

Watoto wanaozaliwa na kina mama waliougua malaria wakati wa ujauzito hua na uzani wa chini. Hii husababisha watoto hawa kuwa katika hatari ya maambukizi tofauti na hata kufa katika mwaka wao wa kwanza.

Wanawake walio katika ujauzito wao wa kwanza wanoishi ktika sehemu ambazo ugonjwa huu umekidhiri hua hawaonyeshi dalili za kawaida zaugonjwa huu.


Sources