Mbona nitahadhari na wanaume waliokomaa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Wasichan wengine huvutiwa na wanaume waliokomaa. Kuwa marafiki na mwanaume aliyekomaa huonekana kama jambo la kusisimua sana, has kama mwanume huyo anajulikana katika jamii, au ana pesa na anaweza kununua vitu. Katika maeneo fulani, mwanaume anayemnunulia mpenzi wake zawadi nyingi hujulikana kama "Baba Sukari".

Mara nyingi, msichana ambaye hushirikiana na mwanaume kama huyu huhisi kuwa ametumiwa kwa ngono tu, au kutendewa maovu, hasa ikiwa mwanaume huyu an mke au ana wanawake wengine wengi.

Wakati mwingine mwanaume aliyekomaa humshinikiza msichana mdogo kushiriki ngono, ikilinganishwa na vijana wa rika lake.

Katika jamii kadhaa, wanawake na wasichana wanaambukizwa virusi vya HIV kushinda kikundi kingine kile. Kuna hatari kubwa kwa wasichana wanaoshiriki ngono na wanaume waliokomaa, kwa sababu wanaume hawa wamekuwa na vipindi vingi ambapo wangeambukizwa virusi vya HIV. Lakini inaweza kufanyika na mwanume wa umri wowote.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020817