Mbona sifai kujilaumu baada ya jaribio la kujiuua
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Uchungu wa kumpoteza mtu aliyejiua husababisha maswali mengi na shaka kubwa.
Fahamu ya kwamba hufai kulaumiwa. Kumbuka kwamba si makosa yako. Ni mpendwa wako aliyefanya maamuzi hayo, sio wewe.
Hatia yahusiana na nia. Ungelijua kwamba mtu huyo alikuwa na nia ya kujiua, ungelifanya uwezalo ili kumzuia.
Kubali kwamba ulifanya uwezalo kutokana na lile ulilojuwa kwa wakati huo. Na ikiwa hukumsaidia kikamilifu na shida aliyokuwa anaipitia kwa wakati huo, elewa ya kwamba binadamu hukosa. Wewe ni binadamu. Haikuwa kimakusudi.
MUHIMU: Unapohisi kujiua kutokana na huzuni, kubali kuwa unapitia sehemu ambayo ni ya kawaida na hueleweka. Lakini tafadhali mhusishe mtaalamu mara moja unapopatwa na mawazo ya kujiua.