Mbona wanawake wengine huavyaa mimba
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Sio jambo rahisi kuamua kuavyaa mimba. Baadhi ya dini hufundisha kuwa ni vibaya kuavyaa mimba, na katika mataifa mengi kuavyaa mimba sio salam wala halali. Kuna sababu nyingi ambazo mwanamke atajaribu kuavyaa mimba. Hapa kuna mifano:
Uja uzito ambao haujapangwahufanyika wakati ambapo:
... mwanamke na mpenzi wake hawajui jinsi uja uzito hufanyika. ... wahudumu wa afya hudhani kuwa wanawake wengine ni wachanga sana kutumia njia za kupanga uzazi. ... wanawake hulazimishwa kushiriki ngono. ... mbinu za kupanga uzazi hazipatikani, hazitumiki vizuri au hazifanyi kazi.
MUHIMU: Mwanamke ambaye ameshirkingono katika muda wa siku 3 zilizopita anaweza kuzuia kushika mimba ikiwa atafanya mambo haraka.