Migogoro ipi ya kawaida inayohusishwa na kujamiiana au ngono
Wanaume wengine hawataki wake zao kutumia njia za upangaji uzazi - kwa sababu huwa hawajui jinsi njia hizo tofauti hufanya kazi. Sababu nyingine inaweza kuwa kuogopa vile afya wa wake wao itakavyokuwa kwa sababu wamesikia hatari za kutumia mbinu hizo, wanaogopa ikiwa wake wao watatumia mbinu hizo huenda wakajamiiana na wanaumme wengine, au wanaweza fikiria kuwa mtu ni mwanamume halisi ikiwa atakuwa na watoto wengi.
Ndoa za kupangwa ni za kawaida kwa nchi nyingi. Bibi na bwana harusi huwa hawana neno la kusema kuhusu ndoa hiyo na kutotakana na ndoa hiyo wasichana wadogo hutengwa na familia zao. Katika jamii nyingi mwanamke huwa mali ya mwanamume ambaye baada ya ndoa huamini kuwa yuko na haki ya kutumia mwili wake kwa raha yake jinsi anavyotaka.
Kutokana na hali hii, wanawake hushindwa kuwapenda waume wao na kufurahia tendo la ngono. Badala yake wao huhisi kana kwamba wameshinikizwa kujamiiana na mtu ambaye hawamjui vyema au kumpenda. Wanaweza kuwakataa waume wao au kutafuta vijisababu kwanini hawataki kujamiiana na waume wao.
Hili likitendeka, waume hukasirika na kuwalazimisha kujamiiana, swala hili hufanyika tena na tena, mwanamke kukataa kujamiiana na mumeo na mumeo kulazimisha tendo la ngono.
Wanaume wengine walio na wake hufikiria kuwa wako na haki ya kujamiiana na wanawake wengine wakati wanaotaka ilihali wake wao ni wao pekee.