Migogoro ipi ya kawaida kwa watoto
Katika nchi nyingi wanawake hawadhaminiwi na kuheshimiwa na familia zao. Katika familia nyingi haswa katika nchi zinazoendelea hupendelea watoto wa kiume kushinda wasichana kwa sababu vijana hutarajiwa kusaidia wazazi wao wanapozeeka. Kwa hivyo familia huwa tayari kuwasaidia watoto wa kiume na huduma za matibabu na elimu kuliko wasichana. Wanawake hawakubaliani na itikadi hizi, wanataka maisha mazuri kwa wasichana wao na wako tayari kwenda kinyume na tamaduni hizi na kuzungumza na waume wao jinsi ya kuwalea na kuwaelimisha watoto wao wote bila kuangalia jinsia.
Kutokana na imani hii iliyotamba kwamba wasichana ni mzigo kwa familia na jamii zao, na licha ya kwamba imani hii imekataliwa na sheria duniani, katika familia nyingi wanawake hushurutisha kuavyaa mimba mimba ya mtoto wa kike au hata kuwaua watoto wa kike kwa kuwanyima chakula na vitu vingine muhimu kama matibabu. Huko India, kwa mfano wapatao watoto wa kike 750, 000 hutolewa kila mwaka kwa hivyo inakuwa vigumu kwa mwanamke kuokoa mtoto wa kike.
Shinikizo kwa wanawake kupata watoto wa kiume katika nchi zinazoendelea ni la kushtua na wanawake wasiozaa watoto wa kiume huwa wanatendewa mabaya na ( waume, mashemeji hata familia zao) wanateswa au hata kufukuzwa kwa nyumba.
Angalau wanafanywa kuwa na hatia na hadhi yao katika familia hupungua.