Mihadarati na Pombe inawezaje kusababisha madhara ya kudumu kwa afya yangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Watu wanaotumia pombe na mihadarati hugonjeka kwa mara nyingi zaidi na ugonjwa huwa mkali kuliko huo wa watu wasiotumia mihadarati na pombe.

Hawa watu wana uwezekano zaidi wa kuwa na:

  • lishe mbovu itakayosababsiha magonjwa zaidi.
  • saratani na shida za moyo, maini, tumbo, ngozi, mapafu na mfumo wa mkojo na hata kuvidhuru viumbe hivyo kwa muda wa kudumu.
  • uharibifu wa ubongo ama mshtuko (kama wanaopata wagonjwa wa kifafa)
  • Kwa wenye wana virusi vya UKIMWI, husababisha ugonjwa yanayoibuka baada ya kupata UKIMWI kuadhiri mgonjwa kwa haraka zaidi.
  • kusahau sahau- kutoweza kukumbuka vitu vilivyofanyika unapoamka.
  • shida za kiakili kama huzuni na wasiwasi ya kudumu ama kuota njozi yaani kuona vitu/watu au kusikia sauti visivyokuwa, kushinda akishuku watu wengine na kukumbuka vitu vilivyomfanyikia kwa siku za nyuma.
  • hufa kwa sababu ya kutumia pombe na mihadarati kupita kiasi.

Pia, majeraha ama kifo kutokana na ajali hufanyika zaidi kwa watu wanaotumia pombe na mihadarati (na hata famiia zao). Hii ni kwa sababu ya kufanya maamuzi mabaya na kufanya vitu vinavyowaweka kwa hatari zaidi usiohitajika na kufanya vitu bila kufikiria kikamilifu wanapotumia pombe au mihadarati. Wakishiriki katika ngono bila kinga, kutumia sindano moja wakijidunga dawa za kulevya au kushiriki ngono ndiyo wapate mihadarati wako hatarini- wanaweza kupata homa ya manjano, UKIMWI na magonjwa mengine ya sehemu za siri.

Watu wanaotafuna tumbaku wako hatarini kupata magonjwa mengi ambayo hudhuru wanaovuta sigara.

Kutafuna tumbaku na bobo kwa mara nyingi husababisha shida za meno na ufizi na vidonda mdomoni, saratani ya mdomo na koo, na shida zingine mwilini wote. Miraa inaweza sababisha shida tumboni na choo yabisi. Dawa za kulevya za kutafuna zaweza sababisha utegemezi.

Watu wengi masikini haswa vijana ambao ni chokora, huvuta gundi na kemikali za aina ya "solvent" ili wasihisi njaa. Tabia hii inaweza sababisha uraibu na shida mbaya zaidi za kiafya kama vile kupata shida katika kuona, kufikiria na kukumbuka, kuvurugana, kupoteza fahamu au hisia za mwili, kukonda sana na moyo kuacha kupiga au kifo.

Matumizi yoyote ya dawa za kulevya ni hatari kama:

  • unaendesha gari, unatumia mashini/mashine au kutumia chombo kinachoweza kukuumiza.
  • una mimba au unanyonyesha.
  • unawashugulikia watoto wachanga.
  • unachukua dawa haswa ya kupunguza uchungu, kufanya ulale, mshtuko (yaani "seizures") au ya kutibu ugonjwa wa ubongo.
  • una ugonjwa wa ini au figo.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010306