Mwili wangu utabadilika vipi wakati wa kubalehe

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Wasichana wote hupitia mabadiliko mwilini mwao, lakini mabadiliko haya huwa tofauti katika kila msichana. Kwa hiyo usijali kama mwili wako uko tofauti na dadako au rafiki yako.

Kukua Badiliko la kwanza ni kuwa utakua unakua haraka. Labda utakuwa mrefu kuliko wavulana wa umri wako kwa muda. Utaacha kukua mwaka moja hadi mitatu baada ya kuanza kwa hedhi zako.

Mabadiliko ya mwili Licha ya mwili kukua kwa kasi, mwili wako utaanza kubadilika. Kuna kemikali ya asili katika mwili wako iitwayo homoni ambayo hufanya mwili wako kukua na kufanya mabadiliko hayo kutokea.

  • Utarefuka kwa kima na kimzunguko
  • Uso wako utakuwa na mafuta mafuta na kukua kwa alama za chunusi.
  • Utatokwa na jasho zaidi
  • Nywele zitamea kwa makwapa na katika sehemu zako za siri.
  • Matiti yako yatakuwa huku yakiweza kutengeneza maziwa. Titi moja laweza kukua kabla la lingine, lakini titi hilo lengine dogo hukua pia.
  • Uke wako utaanza kutoa majimaji au uchafu wa majimaji.
  • Hedhi zako zitaanza.

Ndani ya mwili Kuna mabadiliko mengine ambayo huwezi kuyaona. Tumbo la uzazi, mishipa, ovari na uke hukua na kubadili nafasi.

Vile unahisi. Unapopitia mabadiliko haya, unapata kuelewa mwili wako. Unaweza kuvutiwa na wanaume na kwa marafiki zako. Kunaweza kuwa na wakati ambapo hisia zako zitakushinda kuzidhibiti. Katika siku kabla ya hedhi zako ni kawaida kuwa na hisia nzito za kila aina--kwa mfano:-furaha, hasira wasiwasi.

Hedhi. Kutokwa na damu kila mwezi ni dalili kwamba waweza kupata mimba. Hakuna msichana anayejuwa siku kamili ya kupata hedhi kwa mara ya kwanza. Huwa hutokea baada ya matiti na nywele katika mwili wake zinapokua. Miezi kadhaa kabla ya hedhi za kwanza, anaweza kushuhudia maji maji katika uke wake. Hii ni sawa.

Wasichana wengine hufurahia wanapopata hedhi kwa mara ya kwanza, haswa ikiwa wanajua la kutarajia. Wasichana ambao hawajawahi kuambiwa kuhusu hedhi huwa wako na wasi wasi damu ikianza kutoka. Ni jambo ambalo hutokea kwa wanawake wote, na unaweza kukubali au hata kujivunia. Usimruhusu mtu yeyote yule akufanye ufikirie kuwa ni jambo chafu na la aibu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020803