Nafaa kuelewa nini kuhusu kiwewe

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Baada ya mtu kupatwa na kiwewe, anaweza kupatwa na athari tofauti, kama vile:

  • Kurudia tukio lililoleta kiwewe mara kwa mara akilini mwake. Wakati yuko macho, anaweza kukumbuka matukio mabaya yaliyotendeka. Wakati wa usiku, anaweza kupata ndoto za matukio hayo, au atashindwa kupata usingizi kwa vile anafikiria kuhusu matukio hayo.
  • Wakati mwingine hana hisia zozote. Huenda akawaepuka watu au mahali ambapo panamtia kiwewe.
  • Anakuwa mwangalifu sana. Kila mara, anaangalia kuhakikisha kuwa hakuna hatari, anaweza kupata shida kupumzika na kulala. Huenda akashtuka sana.
  • Hisia za hasira au aibu kubwa kuhusu kilichotendeka. Ikiwa mtu aliepuka mkasa ambapo watu wengi walikufa au kupata majeraha mabaya, ataona ni kama ana hatia kwani hakuumia kama wengine.
  • Hisia za kuwa mbali na watu.
  • Kuwa na tabia zisizoeleweka za vurugu, ambapo anachanganyikiwa asijue aliko.
  • Watu wanaopata shida kutokana na kiwewe huwa na wasiwasi au huzuni kubwa, au pia wao hutumia vibaya pombe na mihadarati.

Ishara hizi ni jambo la kawaida katika kukabiliana na wakati mgumu. Kwa mfano, ni jambo la kawaida kuwa na hisia za hasira kuwa mkasa ulitokea, na kuwa mwangalifu ikiwa bado kuna hali ya hatari. Lakini ikiwa ishara hizi ni mbaya hivi kwamba mtu hawezi kuendelea na shughuli zake za kila siku, au ikiwa ishara hizi zitaanza miezi kadhaa baada ya tukio, huenda muathiriwa ana shida za kiakili.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011510