Napaswa kula nini kwa muda ninaonyonyesha

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Akina mama wanastahili kula vyema ili kupata nguvu, kuwalea watoto vyema na kwa kazi wanayoifanya. Wanahitaji kula chakula kilicho na protini, mafuta, matunda na mboga. Wanahitaji kunywa maji mengi pia, maji safi, maziwa, chai ya majani na sharubati ya matunda. Mwili wa mwanamke utateneneza maziwa ya mtoto.

Kula na unywe maji ya kutosha kukidhi njaa na kiu. Usitumie kileo, miraa na dawa zisizohitajika. Maji safi, matunda na sharubati ya mboga, maziwa na chai ya majani ni bora kuliko kahawa chungu na soda.

Watu wengine hudhani kuwa mama ambaye amejifungua hafai kula vyakula fulani. Lakini, ikiwa mama hatakula vyakula vyenye afya, basi anaweza kuugua utapiamlo, upungufu wa damu mwilini na magonjwa mengine.

Wakati mwingine akina mama hupewa vyakula maalum wanaponyonyesha. Vitendo hivi ni vizuri, haswa ikiwa vyakula hivi ni vya afya. Vyakula vya afya huusaidia mwili wa mwanamke kukua ukiwa wa nguvu na afya, haraka baada ya kujifungua.

Mwanamke anahitaji chakula cha dharura ikiwa:

  • anawanyonyesha watoto 2.
  • anamnyonyesha mtoto mmoja huku akiwa mja mzito.
  • watoto wake wameachana kwa muda wa chini ya miaka 2.
  • anaugua au hana nguvu.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010805