Naweza kuwa na uhusiano wa kuridhisha kingono

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Watu wengi wanaamini kwamba wanawake walio na ulemavu hawawezi kuwa, au hawapaswi kuwa na, hisia za ngono. Hawatarajiwi kuwa na tamaa ya kimapenzi au kuwa wazazi. Lakini wanawake walio na ulemavu huwa na hamu ya kimapenzi na uhusiano wa ngono kama mtu mwingine tu. 

Ikiwa ulizaliwa na ulemavu, au ilitokea ulipokuwa kijana, unaweza kuwa na wakati mgumu kuamini wewe unavutia kingono. Kuzungumza na wanawake wengine ambao wako na ulemavu kuhusu hofumyao wenyewe, na jinsi wanavyokaniliana na hali hio, ni njia bora ya kujifunza kujihisi tofauti wewe mwenyewe. Lakini kumbuka kuwa na subira. Inachukua muda kubadili imani uliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

Ikiwa wewe ni mwanamke aliye na ulemavu wa hivi karibuni, unaweza kuwa ulizoea kufikiri kuwa wewe ni mzoefu katika maswala ya ngono. Lakini unaweza kutojua kwamba unaweza kuendelea kufurahia ngono. Unaweza fikiria kwamba huvutii kingono tena na ukahuzunika kwamba kujamiiana sasa kutabadilika. 

Wanawake walio na ulemavu wanaweza kusaidika kwa kusoma taarifa kuhusu kujamiiana ambazo husomwa na wanawake wengine wasio na ulemavu. Jaribu kuzungumzia swala la ngono na wao, walimu unao waamini, wahudumu wa kiafya na wanawake wengine walio na ulemavu.

Wewe na mpenzio mtahitaji kujaribu vitendo vya kuridhishana. Kwa mfano iwapo hauna hisia kwa mikono au sehemu za siri, wakati wa kujamiiana unaweza kupata viungo vingine vitakavyo chipua hisia, kama vile, masikio, matiti, au shingo. Hii inaweza kusaidia iwapo ulemavu umefanya sehemu za uzazi ziziridhie ngono. Unaweza pia kujaribu mitindo kadhaa, kama kulala kwa upande, au kuketi kwa incha ya kiti. Ikiwa wewe na mpenzi wako mnaweza kuzungumza kwa uaminifu, mapenzi ya kuridhisha yanaweza kutokea. Lakini kumbuka sio lazima uridhike na kidogo kuliko upendavyo. Sio lazima ujamiiane na mtu asiyejali maslahi yako.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011110