Nawezaje kuepuka shida za kiakili

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kuepuka_shida_za_kiakili

Mara nyingi, wanawake hawapati muda wa kupumzika kutokana na shughuli zao. Ni jambo la muhimu kila mwanamke aweke shida zake kando wakati mwingine, na afanye apendavyo. Vitu ambavyo sio kawaida wewe kuvifanya - kama vile kuwa na muda wako peke yako, kwenda madukani ya jumla, kufanya kazi kwenye busatani, au kupika na rafiki - kunaweza kusaidia.

Shughuli ambazo hukusaidia kujihisi huru: Ikiwa una hasira, fanya kazi nzito. Kutunga mashairi, nyimbo na hadithi kunaweza kukusaidia ikiwa unaona ugumu kusema mambo fulani kwa watu. Ama unaweza kuchora bila kutumia maneno - sio lazima uwe mchoraji.

Unaweza kuwa na mazingira yenye furaha: Jaribu kukarabati sebule ili ikufae wewe. Hata iwe ndogo vipi, utaona kuna mpangilio na utahisi una udhabiti ikiwa imepangwa kulingana na unavyotaka. Hakikisha kuna mwangaza na hewa safi ya kutosha.

Jaribu kuwa katika mazingira yenye urembo. Unaweza kuweka maua chumbani, cheza miziki, au tembelea mahali panapopendeza.

Zingatia tamaduni ambazo zinakujenga kwa undani: Jamii kadhaa zina mazoezi ambayo husaidia kutuliza akili na mwili, na kujenga nguvu ya undani. Kwa mfano, kuomba, kutafakari na hata mazoezi ya viungo. Mazoezi haya yatakuwezesha kudhibiti hisia za wasiwasi na shida zingine maishani.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011512