Nawezaje kujenga imani kati ya watu au wanachama wa kikundi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kujenga_imani_kati_ya_watu_au_wanachama_wa_kikundi

  • Jaribu kuwa wazi unaposikiliza kila kitu mtu mwngine anasema, bila kutoa hukumu.
  • Jaribu kuelewa hisia za mtu mwingine. Ikiwa umekuwa na tukio sawa na lake, fikiria jinsi ulivyohisi. Jaribu sana usilinganishe tukio la mtu mwingine na lako. Ikiwa humuelewi, usijifanye kuwa unamuelewa. Hkuna watu wawili ambao wapitia matukio sawa maishani. Kuna mengi ya kuelewa kuhusu mtu mwingine.
  • Usimwambie mtu la kufanya. Unaweza kumsaidia kuelewa jinsi misukumo ya familia, jamii na majukumu ya kazini yanaathiri hisia zake, lakini lazima mwenyewe afanye uamuzi.
  • Usidhanie kuwa mwanamke hawezi kusaidika.
  • Heshimu usiri wa mwanamke. Usiwaambie wengine alichokuambia, ila tu iwe ni muhimu kwa kuyalinda maisha yake. Lazima umjulishe kuwa ungependa kuzungumza na mtu mwingine, kwa usalama wake.

Ni rahisi kukibadilisha kikundi kiwe kikundi cha usaidizi, kuliko kuanzisha kikundi kipya. Kuwa mwangalifu unapochagua husiano za usaidizi. Jenga husiano na watu ambao wataheshimu hisia na usiri wako.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011514