Nawezaje kujifunza kujithamini kama niko na ulemavu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Iwapo mwanamke amesaidiwa na familia, shule na jamii kuishi maisha bora iwezekanavyo, hisia zake za kujithamini zitakua juu, iwapo yuko na ulemavu au la. Lakini kama mwanamke atakua akijua kuwa yeye hana thamana kama wengine kwa sababu yuko na ulemavu, Inabidi afanye bidii kujifunza kujithamini. Utaratibu huu si rahisi ila inawezekana kwa kuchukua hatua chache.

Hatua ya kwanza ni kukutana na watu wengine.

Ukijulikana na wanawake wengine, watajua ya kwamba mwanamke aliye na ulemavu na asiye nao hawana tofauti kubwa. Kila uendapo nje itakua rahisi kukutana na kuzungumza na wengine.

Hatua ya pili ni kuanza au kujiunga na kikundi cha wanawake.

Kuongea na wengine kunaweza kukusaidia kutambua uwezo na udhaifu wako. Kikundi hupeana sehemu mwafaka ya mwanamke kuzugumza kwa uhuru-ikiwa mtakubaliana msiseme chocohote nje ya kikundi mnachojadiliana ndani ya kikundi.

Unaweza pia kujiunga au kuanzisha kikundi cha wanawake walio na ulemavu kisha mjadiliane kuhusu changamoto zinazotokana na ulemavu maishani. Mnaweza kusaidiana nyote wakati wa raha na shida.

Mnaweza kusaidiana kujifunza kujitegemea pia. Duniani kote wanawake walio na ulemavu wanafanya kazi kama madaktari, wauguzi, wauzaji katika duka, waandishi, waalimu, wakulima na waandalizi katika jamii. Kwa usaidizi wa kila mtu, unaweza kuanza kujiandaa kwa maisha ya baadaye, kama vile mwanamke mwingine wa kawaida hufanya.

MUHIMU: Angazia yale unaweza kufanya, sio yale huwezi kufanya.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011105