Nawezaje kujikinga na maabukizi ya pepopunda

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kujikinga_na_maabukizi_ya_pepopunda

Maambukizi ya pepopunda huuwa. Mwanamke anaweza kuambukizwa pepopunda wakati viini vinavyoishi kwa kinyesi cha binadamu au wanyama viingiapo mwilini kupitia kwa jeraha.

Ingawa mtu yeyote anaweza kuambukizwa pepopunda, wanawake na watoto wamo hatarini haswa wakati wakujifungua.

Waweza kuambukizwa pepopunda ikiwa kifaa kinachotumiwa na daktari hakijachanjwa na kuingizwa katika nyumba ya mtoto tumboni au kutumika kukata kitovu cha mtoto na mama.

Ili kuzuia pepopunda, wasichana wote na wanawake waja wazito wanahitaji kuchanjwa dhidi ya Pepopunda. Kama mwanamke ni mja mzito na hajachanjwa, anastahili kudungwa sindano wakati anapotembelea kwa mara ya kwanza kliniki ya wanawake waja wazito na kudungwa chanjo nyingine baada ya mwezi mmoja. Halafu ikiwezekana anastahili kufuata ratiba ifuatayo:

Chanjo ya tatu: angalau miezi sita baada ya chanjo ya pili Chanjo ya nne: angalau mwaka mmoja baada ya chanjo ya tatu Chanjo ya tano: angalau mwaka mmoja baada ya chanjo ya nne Kisha awe anapewa chanjo kila baada ya miaka kumi.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010211