Nawezaje kuzuia kufura kwa viungo vya tumbo ya uzazi Prolapse

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kuzuia_kufura_kwa_viungo_vya_tumbo_ya_uzazi_Prolapse

Ikiwa mwanamke amekuwa mjamzito mara kadhaa, au kuhisi uchungu kupita kiasi wakati wa kujifungua au kujifungua mapema, misuli na mishipa inayoshikilia uzazi wake yaweza kuwa dhaifu.

Hii inaposhuhudiwa tumbo la uzazi laweza kuanguka hadi katika uke. Hii inaitwa prolapse au kufura kwa tumbo la uzazi.

Dalili ya prolapse inaweza kuwa kuvuja au kudondoka kwa mkojo. Nyakati zingine mfuko wa uzazi waweza kuonekana katika njia ya uke. Kuzuia hayo, unashauriwa kuwacha angalau muda wa miaka miwili kila baada ya kujifungua mtoto. Unapowadia wakati wa kuhisi uchungu wa kuzaa, sukuma mtoto wakati njia ya uzazi imefunguka na ikiwa kuna haja ya kusukuma mtoto. Usimruhusu mtu yeyote yule kusukuma tumbo lako chini ili mtoto atoke haraka.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010209