Nawezaje kuzuia kukakamaa na kuweka misuli yangu kuwa na nguvu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ili kuzuia ukakamavu, na kuweka misuli yako kuwa na nguvu, unahitaji kupata mtu ambaye anaweza kukusaidia kufanya mazoezi ya mikono na miguu yako kila siku. Jaribu kuhakikisha kwamba kila sehemu ya mwili wako inatembea. Kama ulikuwa na ukakamavu kwa miaka mingi, itakuwa vigumu kabisa kunyoosha viungo vyako. Lakini mazoezi hayo kuzuia ukakamavu kuzidi kuwa mbaya na yanaweza kufanya viungo vyako kulainika kidogo, kidogo na kuweka misuli yako kuwa na nguvu.

MUHIMU: Ikiwa uungo umejikunja kwa muda mrefu, kuwa mpole. Usijaribu kuukunjua kwa nguvu mara moja.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011109