Nawezaje kuzuia matatizo ya ngozi
Jaribu kusonga angalau baada ya kila masaa mawili. Kama wewe hulala chini kila wakati kuwa na mtu wa kukusaidia kubadili namna unavyo kaa.
Lala au keti juu ya sakafu laini ambayo itapunguza shinikizo kwenye viungo vigumu. Cushoni au pedi za kulalia husaidia sehemu za nje zilizo na viungo vigumu. Au tengeneza cushoni rahisi au pedi ya kulalia kutokana na mifuko ya plastiki iliyoo jazwa na makapi ya maharagwe au mpunga. Ni lazima ijazwe upya kila baada ya mwezi mmoja.
Chunguza mwili wako wote kwa umakini kila siku. Unaweza ukatumia kioo kujitazama mgongoni. Ikiwa utaona sehemu nyeusi au nyekundu, usilale tena kwa upande huo hadi ngozi yako itakaporejea katika hali ya kawaida.
Jaribu kula mboga na matunda kwa wingi na vyakula vilivyo na protini.
Wakati wa hedhi usitumie nguo au tampons ndani ya sehemu za uzazi ili kunasa damu. Huenda zikabana mifupa kutoka upande wa ndani na kusababisha vidonda katika sehemu ya uzazi.
Jaribu kuoga kila siku. Kausha ngozi yako lakini usiikwaruze. Usitumie aina yoyote ya mafuta ya kujipaka yanayo lainisha ngozi, kwa sababu yatafanya ngozi yako kuwa laini na dhaifu zaidi. Usitumie kileo kwa ngozi yako.