Nawezaje kuzuia shida za kiafya kwa kujenga husiano

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nawezaje_kuzuia_shida_za_kiafya_kwa_kujenga_husiano

Inasaidia sana ukiwa na mtu wa kuzungumza naye. Katika uhusiano wa kusaidiana, watu wawili au zaidi huamua kujuana na kuelewana. Hii inaweza kufanyika katika aina yoyote ya uhusiano - kati ya marafiki, watu wa familia moja, au wanawake wanaofanya kazi pamoja, au katika kikundi ambacho hukutano kwa mambo tofauti. Pia, kikundi kipya kinaweza kuundwa kwa sababu watu wana shida aina moja. Vikundi hivi huitwa, "vikundi vya msaada".

Kwa watu wawili wanaofahamiana vyema, uhusiano wa kusaidiana huanza polepole, kwa sababu watu husita kuzungumzia shida zao. Inachukua muda kwa wasiwasi hii kuisha na kuanza kumuamini mtu tena.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011513