Ni Sababu zipi husababisha mabadiliko ya hedhi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_Sababu_zipi_husababisha_mabadiliko_ya_hedhi

Ni hali ya kawaida kwa hedhi kubadilika mara kwa mara kutokana na sababu kama ugonjwa, dhiki, ujauzito, kunyonyesha, kusafiri safari ndefu, kufanya kazi kupita kiasi, ama kubadili mlo. Ila mfumo wa hedhi ukibadilika ghafla, kuchelewa kwa miezi kadhaa, au kuambatana na shida nyingine, huenda ikawa ni ishara ya tatizo kubwa.

Ikiwa siku za hedhi zitabadili mfumo ghafla, kila wakati inapaswa ufikirie uwezekano wa kupatwa na ujauzito wakati wowote- licha ya kutumia njia ya upangaji uzazi.

wakati mwingine Ovari haitoi yai. Wakati jambo hili linapotokea, mwili unapunguza kiwango cha hedhi, ambacho husababisha mabadiliko ya mara ngapi au kiasi gani mwanamke hutokwa na damu. Wasichana ambao hedhi zao ndio zinaanza- au wanawake ambao hivi karibuni wamesimamisha kunyonyesha-wana uwezekano wa kutokwa na damu kwa muda wa miezi michache, au kupata kiwango kidogo cha kutokwa na damu, au kuongezeka kutokwa na damu. Hedhi zao hurudi za kawaida baada ya mud fulani.

Wanawake ambao hutumia homoni kama njia ya upangaji uzazi mara nyingine hupata hedhi katikati ya mwezi.

Wanawake wenye umri mkubwa ambao hawajafika kikomo kupata hedhi wanao uwezekano wa kupata hedhi inayoambatana na utokaji mwingi wa damu au kutoka kwa damu mara kwa mara kuliko wakati wa ujana wao. Wanapokaribia uzee, huenda wakakosa kupata hedhi kwa muda wa miezi michache ndipo wapate hedhi tena.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010217