Ni hatua gani huchukuliwa wakati wa uchunguzi wa chungu cha uzazi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_hatua_gani_huchukuliwa_wakati_wa_uchunguzi_wa_chungu_cha_uzazi

Mhudumu wa afya atachunguza sehemu zako za siri, na kuangalia ndani ikiwa kuna uvimbe, matuta, vidonda, au mabadiliko katika rangi.

Kwa kawaida, mhudumu wa afya ataweka kifaa kiitwacho, speculum kwenye uke wako. Speculum ni kifaa kidogo cha chuma kinachotumiwa kuuweka uke wako wazi. Kisha, atachunguza kuta za uke na njia ya uzazi kwa uvimbe, matuta, vidonda, au kutokwa. Unaweza kuhisi shinikizo kidogo au usumbufu wakati speculum inawekwa ndani, lakini haitakuumiza. Uchunguzi huu ni huenda vizuri ikiwa misuli yako imetulia na kibofu chako hakina mkojo.

Ikiwa kliniki ina huduma za maabara, mhudumu wa afya atafanya uchunguzi wa magonjwa ya zinaa, ikibidi. Pia, mhudumu wa afya anaweza kufanya uchunguzi kuona ikiwa kuna mabadiliko katika njia ya uzazi, ambayo yanaweza kusababisha saratani. Uchunguzi huu unaweza kuwa aina ya Pap Smear, kuangalia njia ya uzazi kwa macho tu, au uchunguzi mpya wa ugonjwa wa HPV, virusi vinavyosababisha saratani ya njia ya uzazi. Uchunguzi huu hauna maumivu, na hufanywa ile speculum ikiwa mahali ilipowekwa. Ikiwa utapatikana na saratani na kupata matibabu mapema, unaweza kupona.

Baada ya mhudumu wa afya kuondoa ile speculum, atavaa glavu safi kwenye mkono mmoja na kuingiza vidole viwili vya mkono mmoja kwenye uke wako. Atatumia mkono huo mwingine kufinya pande ya chini ya tumbo lako. Hii itamwezesha kujua ukubwa, umbo na mahali ambapo tumbo la uzazi, mirija na ovari zilipo. Uchunguzi huu hauna maumivu yoyote. Ikiwa utapata maumivu, mweleze. Inamaanisha kuwa kuna shida fulani.

Kuna shida zingine ambapo itamlazimu mhudumu wa afya kufanya uchunguzi wa njia ya haja kubwa. Kidole kimoja huingizwa kwenye njia ya haja kubwa na kidole kingine kwenye uke wako. Hii itampa mhudumu wa afya habari zaidi kuhusu shida za uke wako, tumbo la uzazi, mirija na ovari.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010205