Ni mabadiliko gani hufanyika mwilini na magonjwa yapi huja kwa sababu ya dhiki

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ni_mabadiliko_gani_hufanyika_mwilini_na_magonjwa_yapi_huja_kwa_sababu_ya_dhiki

Mtu anapohisi dhiki, mwili hujitayarisha kwa mapambano dhidi ya dhiki. Baadhi ya mabadiliko ambayo hutokea ni:

  • moyo huanza kupiga haraka
  • shinikizo la damu huongezeka
  • mtu huanza kupumua haraka
  • chakula husyagika pole pole

Ikiwa dhiki hii imekuja ghafla na ni ya kutatanisha, mwanamke huhisimabadiliko haya mwilini. Mara dhiki hii inapokwisha, mwili wake hurudia hali yake ya kawaida. Lakini ikiwa dhiki hii sio ya kutatanisha na inafanyika polepole, huenda hatatambua jinsi dhiki inavyouathiri mwili wake, ingawa ishara bado zipo.

Dhiki ambayo huendelea kwa muda inaweza kuonekana na kutambulika kama wasiwasi na huzuni kubwa, kuumwa na kichwa, shida za tumbo, kukosa nguvu. Baada ya muda fulani, dhiki hii inaweza kusababisha magonjwa kama vile, shinikizo la damu mwilini ambayo inawezakusababisha mshtuko wa moyo au kiharusi.

Katika maeneo kadhaa, matatizo ya kihisia hayatiliwi maanani kama shida zingine. Wakati hili linafanyika, huenda watu wakawa na ishara za nje za kuwa na wasiwasi na huzuni kuliko ishara zingine. Ingawa ni jambo la muhimu kutotilia maanani ishara za nje, ni jambo la muhimu kutambua hisia ambazo husababisa ugonjwa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011511