Ni maoni gani yasiyofaa kuhusu ulemavu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Katika kila wanawake 10 mmoja hupatikana na ulemavu unaotatiza maisha yake ya kila siku. Huenda akawa na ugumu wa kutembea, kuinua, kuona, kusikia au hata kutumia akili yake.

Katika makala haya tuna tumia neno mwanamke aliye na ulemavu baadala ya mwanamke mlemavu. Tunafanya hivyo ili kukumbusha watu ya kwamba, japo ulemavu unaweza kumzuia mwanamke kufanya mambo fulani, bado yeye ni mwanamke kama wengine. Ni mwanamke kwanza.

Haijalishi kisababishacho ulemavu wa mwanamke, anaweza kuwa na uzao kama mwanamke asiye na ulemavu. Anahitaji nafasi ya kuendeleza ujuzi wake kwa ukamilifu.

Tamaduni na itikadi za kikwetu wakati mwingine hutoa maoni potovu kuhusu ulemavu. Kwa mfano huenda watu wakafikiria mwanamke yuko na ulemavu kwa sababu ya jambo fulani alilolifanya zamani na sasa anaadhibiwa. Au wakafikiri ulemavu wake ni wa 'kushika' (kuambukiza) Kwa maantiki hiyo wakaogopa kujumuika naye. "Ulemavu hausababishwi na hatia yoyote afanyayo mtu".

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011102