Ninawezaje kujikinga na matatizo za kiafya

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninawezaje_kujikinga_na_matatizo_za_kiafya

Matatizo mengi ya kiafya yanaweza kuzuiwa (kabla zianze) kwa lishe bora, usafi, mapumziko na kuhakikisha wanawake wanapata mahitaji yao ya msingi.

Jamii zenye afya husaidia wanawake kukaa wenye afya. Wanawake wenye afya wanaweza kutunza familia zao. Familia zenye afya zinaweza kuchangia zaidi katika jamii.

Si rahisi kwa wanawake kujikinga kutokana na magonjwa wakati wote. Ingawa wanawake hufanya jitihada nyingi kuhakikisha familia na jamii zao zina afya bora, huwa ngumu kwa wanawake wengi kupata wakati, nguvu na pesa kutilia maanani kwa mahitaji yao ya kibinafsi kiafya. Kwa vile wanawake wamefundishwa kutanguliza mahitaji ya wengine kwanza, huwa wanabaki na muda mchache kwa ajili yao binafsi, baada ya kutunza familia zao. Na mara nyingi rasilimali ya nyumbani huwa pungufu na hutumiwa kukidhi mahitaji ya watoto na wanaume kwanza.  

Hata hivyo, kwa muda ujao, inaokoa uchungu mwingi na matatizo za kiakili kujiepusha na shida za kiafya kabla zianze badala ya kuzitibu baadaye. Baadhi ya vitu hivi havihitaji muda au pesa. Zingine huchukua muda wa ziada, nguvu na pesa - tu mwanzoni. Lakini kwa vile kujikinga kunajenga afya na nguvu ya mwanamke na familia yake, jamii yake, maisha utakuwa rahisi na bora zaidi baadaye.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010202