Nini husababisha ulemavu
From Audiopedia
Katika nchi maskini, ulemavu mwingi husababishwa na umaskini, ajali na vita.
Kwa mfano:
Iwapo mwanamke hapati chakula chakutosha akiwa mjamzito, huenda mwanawe akazaliwa na ulemavu. (ulemavu wa kuzaliwa).
Iwapo mtoto hapati chakula kizuri cha kutosha anaweza kuwa kipofu au ulemavu wa akili.
Mazingira machafu na maeneo yaliyojaa watu kupindukia, pamoja na ulaji mbaya na ukosefu wa huduma muhimu za afya na chanjo, husababisha aina nyingi za ulemavu.
Katika vita vya siku hizi, wanawake wengi zaidi huuliwa au kulemazwa zaidi ya wanajeshi na wanaume wengine.
Lakini kama sababu hizi za ulemavu zingeondolewa, bado kutakuwepo na watu walio na ulemavu- ni sehemu ya kimaumbile ya maisha.