Nini la muhimu kufahamu kuhusu wasiwasi
From Audiopedia - Accessible Learning for All
QR for this page
Jina lingine la wasiwasi ni "dhiki".
Kila mtu huwa na hisia za wasiwasi mara kwa mara. Hisia hizi husababishwa na tukio fulani, na hutokomea baadaye. Lakini wasiwasi hii inapoongezeka na kuwa mbaya, au ikija bila sababu, basi kuna uwezekano kuwa ni shida ya kiakili.
Ishara:
Hofu ni aina ya wasiwasi mbaya. Huja bila kutarajiwa na inaweza kukaa kwa muda wa dakika chache hai masaa kadhaa. Zaidi ya ishara hizi, mtu huwa na hisia za hofu ya kushambuliwa, na kuogopa kuwa huenda akapoteza fahamu au kufa. Pia ataumwa na kifua, awe ugumu wa kupumua na kuhisi kuwa kuna jambo baya linaenda kutendeka.