Nitawezaje kupumzika

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitawezaje_kupumzika

Pumzika

Wanawake wengi hufanya kazi za kupika, kubeba maji na kutafuta kuni ili kusaidia familia zao. Ikiwa mwanamke anafanya kazi zingine mbali na za nyumbani, basi huwa na mzingo maradufu. Anaweza kuwa anafanya kazi kiwandani, ofisini, au shambani na anaporudi nyumbani anaendelea na kazi yake ya pili ya kuitunza familia. Hizi kazi zote zinaweza kusababisha uchovu, utapiamlo na ugonjwa, kwa sababu mwanamke yule hana wakati wa kupumzika au kupata chakula cha kutosha cha kumpa nguvu za kufanya kazi zake.

Ili kupunguza kazi anazofanya, familia inaweza kushirikiana kwa kazi za nyumbani. Kupika, kuosha, kutafuta kuni na kuteka maji pamoja na wanawake wengine (kwa pamoja au kwa zamu) inaweza kurahisisha kazi za mwanamke. Ikiwa anafanya kazi ya kulipwa au la, huenda atahitaji usaidizi kuwalea watoto wake. Baadhi ya wanawake huwa na makundi ya kuwalea watoto, ambapo mwanamke mmoja anawachunga watoto ili wanawake wengine waeanya kazi. Kila mwanamke humlipa yule mwanamke ambaye anawachunga watoto au wanafanya hivi kwa zamu.

Ikiwa mwanamke ni mja mzito, anahitaji kupumzika zaidi. Anaweza kuelezea familia yake umuhimu wa yeye kupata kupumzika, na kuwashawishi wamsaidie kwa kazi zingine.

Mazoezi Wanawake wengi hufanya mazoezi wanapofanya kazi zao za kila siku. Lakini ikiwa mwanamke atakaa mahali pamoja anapofanya kazi-kwa mfano, ikiwa yeye huketi au kusimama mchana kutwa kiwandani au ofisini-ni muhimu sana kwake kutembea na kujinyoosha kila siku. Hii itasaidia kufanya moyo, mapafu na mifupa kuwa yenye nguvu. Ikiwa kazi yako ni ya kukaa au kusimama kwa masaa mengi, unaweza kupata matatizo ya kiafya. Wakati mwingine, magonjwa haya hudhihirika baada ya miezi au miaka kadhaa. Nyingi ya shida hizi zinaweza kuepukwa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010203