Saratani ni nini

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Saratani ni ugonjwa hatari ambao unaweza kuathiri kiungo chochote cha mwili. Ikiwa utapata matibabu haraka, unaweza kupona, lakini ukikawia bila kupata matibabu, husababisha kifo. Watu wengi hufa wanapougua saratani, hasa wanapokosa kupata matibabu.

Viumbe vyote, kama mwili wa binadamu, umetengenezwa kwa nyingi ndogondogo, ambazo ni vigumu kuziona labda utumie darubini. Wakati mwingine seli hizi hubadilika na kumea visivyo, na kusababisha vimelea. Baadhi ya vimelea hutokomea bila matibabu. Lakini vimelea vingine hukua na kuenea na kusababisha shida za kiafya. Vimelea vingi sio saratani, ingawa vingine huwa saratani.

Saratani ya njia ya uzazi, matiti na tumbo ndio kawaida kwa akina mama. Saratani nyingine za kawaida ambazo huwaathiri wanaume kwa wanawake ni saratani ya mapafu, utumbo, maini, mdomo na ngozi.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011402