Vipi mabadiliko kwa maisha yangu na jamii yadhuru afya ya akili yangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Vipi_mabadiliko_kwa_maisha_yangu_na_jamii_yadhuru_afya_ya_akili_yangu

Katika sehemu nyingi duniani, jamii zimelazimika kubadilika ghafla bin vuu - sababu ya mabadiliko ya kiuchumi au sababu ya migogoro ya kisiasa. Mabadiliko mengi huganya familia na jamii kuwajibika na kubadili mienendo yao ya kimaisha.

Mfano:

"Jina langu ni Edhina. vita vilipoanza, jeshi walikuja na kulazimisha wanaume wa kijiji chetu kupigana. Wanawake wengine walibakwa. Tulikimbia milimani, lakini ilikuwa vigumu kupata chakula. Sasa tunaisha kama wakimbizi kwa iliyoko mpakani. Tunapata chakula cha kutosha, lakini watu wengi ni wagojwa. Kambi imejaa wageni. Kila siku hushangaa- ikiwa nitawahi kuona kwetu tena?"

"Jina langu ni Jurema. Kila mwaka, ardhi yetu ilitoa mavuno kidogo. Ilitubidi tukopeshe pesa kununua mbegu, na hata kujaribu kununua mbolea, lakini tulishindwa kupanda vya kutosha kuweza kulipa benki pesa zao. Mwishowe, tulilazimishwa kutoka kwa ardhi yetu. Kwa sasa tunaishi kwa kibanda nje ya mji. Kila asubuhi niamkapo, huskiza ndege wanavyoamkua asubuhi. Kisha hukumbuka- hamna ndege huku. Ni siku nyingine ya kusugua sakafu za watu. "

Familia na jamii zikisambaratika, au maisha yanapobadilika mno hadi miondoko ya kizamani yakakosa kufanya kazi, watu huweza kuwa na shida za kiakili.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011505