Wanawake wagani wako na uwezekano mkubwa wa kudhalilishwa
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Kwa wapenzi wengi, mwanamume huwa na vurugu zaidi kwa mara ya kwanza wakati mwanamke ni mjamzito. Huweza kuhisi kana kwamba anapoteza mamlaka kwa sababu hawezi kudhibiti mabadiliko katika mwili wa mpenzi wake. Anaweza kuhisi hasira kwa sababu mwanamke amepea kipaumbele kwa mtoto kuliko mwanamume, au kwa sababu mwanamke hatataka kujamiiana na mpenziwe. Pia, wapenzi wengi huwa na wasiwasi kuhusu suala la pesa wanapotarajia mtoto mchanga.
Wanawake walio na ulemavu pia wako na uwezekano mkubwa wa kudhalilishwa: Wanaume wengine wanaweza kushikwa na hasira kwa sababu hawakupata mwanamke 'kamili'. Wanaume hufikiria kwamba ni rahisi kumkalia mwanamke aliye na ulemavu kwa sababu anaweza kushindwa kujitetea.