Je kuna dhana zipi jinsi wanaume huwaumiza wanawake

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Je_kuna_dhana_zipi_jinsi_wanaume_huwaumiza_wanawake

Click Code to Download

Hizi hapa ni miongoni mwa dhana ambazo watu huwa nazo:-

"Mwanamume anaweza kumtendea chochote mkewe. " Ukweli: Hakuna mwanamume yeyote aliye na ruhusa ya kumchapa mkewe. Hakuna chochote ambacho mwanamke atakofanya kitakachompa mwanamume haki ya kumpiga, hata kama kwa maoni yake anastahili kupigwa - au hata kama mwanamke anaona anastahili kupigwa.

"Ni kwa sababu yeye hulewa. . . " Ukweli: Pombe haisababishi vurugu, lakini huifanya kuwa mbaya zaidi. Vurugu ni jambo la kawaida hata miongoni mwa watu wasiotumia vileo.

"Hangempiga, kama hangempenda sana. " Ukweli: Kumpiga mtu sio ishara ya upendo. Mapenzi ni kuonyeshana heshima na ukarimu.

"Ni mambo yao hayo. Sio vizuri kuingilia mambo ya wanandoa. " Ukweli: Vurugu sio tu jambo la kifamilia. Wanawake wengi huumizwa au kuuawa. Vurugu ni shida ya kijamii na kiafya.

"Ni wanaume maskini na ambao hawajasoma, ambao huwachapa wake wao. " Ukweli: Vurugu sio shida tu ya kutojua kusoma wala umaskini. Vurugu inaweza kutokea katika familia yoyote: matajiri au maskini, waliosoma na wale hawajasoma, mjini au mashambani.

"Afadhali watoto wakae na baba yao. Anaweza kuwalea vyema. " Ukweli: Sio vizuri kwa familia mwanamke anapoendelea kukaa na mwanamume mwenye vurugu. Mwanamume huyo anawafundisha watoto njia mbovu za kukabiliana na hisia zao, na jinsi wanawake wanastahili kutendewa. Sio vizuri kama anampiga mama na watoto wake.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020104