Kuna umuhimu gani kumuona daktari au muuguzi wa afya ikiwa nitahisi kujiua

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Kuna_umuhimu_gani_kumuona_daktari_au_muuguzi_wa_afya_ikiwa_nitahisi_kujiua

Click Code to Download

Unyogovu usiotibiwa ni mojawapo ya sababu kuu ya watu kujiua. Hata matukio ambayo mwanzoni husababisha furaha - kama kupata mtoto au kupata ajira/kazi -yaweza kusababisha unyogovu. Unyogovu baada ya kupata mtoto kwa mfano, kawaida hushuhudiwa. Kati ya wanawake watano, mmoja wao huwa na unyogovu baada ya kujifungua mtoto- wengi wao hukosa kufahamu.

Unyogovu husababishwa na kutosawazishwa kwa kemikali akilini. Ni ugonjwa. Kwa hivyo, haufai kuhisi kama uko na hatia au umekosa sababu ya unyogovu.

Kimsingi, Ikiwa umekuwa ukitaka kujiua kwa muda wa wiki mbili au zaidi, bila shaka uko na unyogovu na unahitaji matibabu. Tafadhali jua siku utakayo muona daktari wa akili, au mtaalamu, ndiposa uchunguzwe kwa ukamilifu. Unyogovu unaweza tibiwa na mchanganyiko wa madawa ya kusawazisha hisia zako, na kupewa mawaidha na mtaalamu wa akili.

Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020911