Kwa nini magonjwa ya zinaa ni shida kubwa kwangu

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Kwa_nini_magonjwa_ya_zinaa_ni_shida_kubwa_kwangu

Click Code to Download

Wanaume na wanawake wanaweza kupata magonjwa ya zinaa. Lakini ni rahisi kwa mwanamke kupata kutoka kwa mwanamume ikilinganishwa na mwanaume kupata kutoka kwa mwanamke. Hii ni kwa sababu uume huingia katika sehemu zingine za mwili wa mwanamke-kama uke, mdomo, au tundu la haja kubwa-wakati wa kujamiiana au ngono. Ikiwa mpira (Kondomu) hautatumika, basi shahawa (semen) ya mwanamume, ambayo yaweza kuwa na maambukizi, ikabaki ndani ya mwili ya mwanamke. Hii humpa mwanamke nafasi kuu ya kupata maambukizi katika tumbo la uzazi, mishipa na ovari. Wakati mwanamke anapokuwa na vidonda kwenye sehemu ya siri wake au mwasho kutokana na maambukizi kwenye uke, anaweza kupata virusi vya ukimwi kwa haraka.

Kwa sababu magonjwa mengi ya zinaa yamo ndani ya mwilili wa mwanamke, dalili ya magonjwa ya zinaa kwa mwanamke ni vigumu kuziona ikilinganishwa na kwa mwanamume. Basi ni vigumu kujua ikiwa mwanamke yuko na maambukizi kwenye sehemu zake za siri-haswa kujua aina kamili ya maambukizi aliyonayo.

Inaweza kuwa vigumu kwa mwanamke kujikinga na magonjwa ya zinaa. Kawaida, lazima ashiriki ngono na mpenzi wake akitaka. Anaweza kukosa kujua ikiwa mpenzi wake hushiriki ngono na wanawake wengine au ikiwa yuko na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Iwapo anaye mpenzi mwingine huenda akamwambukiza mkewe.

Mwanamke anaweza kushindwa kumshawishi mpenzi wake kutumia mpira (kondomu). Kondomu za mpira ni bora zaidi kwa wapenzi, lakini mwanamume ni sharti akubali kutumia.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010503