Kwa nini mimba ya mapema yaweza kuwa hatari kwangu

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Kwa_nini_mimba_ya_mapema_yaweza_kuwa_hatari_kwangu

Click Code to Download

Miili ya wasichana wengi haiko tayari kwa kujifungua salama.

Wasichana wengi wako katika hatari ya kushikwa na hali iitwayo pre-eclampsia, ambayo inaweza kusababisha kifafa wakati wa uja uzito.

Kwa vile miili yao haijakomaa na haiwezi kustahimili kujifungua, akina mama wa umri chini ya miaka 17 wako katika hatari ya kuwa na muda mrefu wa uchungu wa uzazi, au kushindwa kujifungua. Mama yeyote ambaye atapata shida hizi na asipate usaidizi wa mhudumu wa afya, hufa. Kushindwa kujifungua huharibu sehemu ya uzazi, na kusababisha shida ya kutokwa na mkojo na haja kubwa.

Watoto wanaozaliwa na akina mama wa umri chini ya miaka 17 huzaliwa wakiwa na uzani mdogo sana au kabla ya wakati wao.

Ikiwa wewe tayari ni mja mzito, muone mkunga aliyehitimu au mhudumu wa afya haraka iwezekanavyo, ili akueleze jinsi salama ya kujifungua.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020810