Mbona nafaa kujichunga zaidi haswa baada ya mtu kujiua

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Mbona_nafaa_kujichunga_zaidi_haswa_baada_ya_mtu_kujiua

Click Code to Download

Hisia kali za maumivu na hofu kubwa unayohisi baada ya kumpoteza mtu kwa kujiua yaweza kufanya uone ugumu wa kufanya lolote. Ni vigumu sana kuendelea baada ya mtu kujiua. Uponyaji unaweza kuchukuwa muda. Usijaribu kujiharakisha, lakini kuwa na subira na mpole.

Ikiwa ni vigumu kuwa makini, kusahausahau, au unashindwa kuzingatia; tafadhali, fahamu ya kwamba unapitia hisia za mawazo mengi ya kawaida na usijilazimishe sana. Jaribu kupata msaada wa masuala yako ya kila siku. Kazi ndogo yaweza kuonekana balaa, kwa hivyo tafuta msaada wakati unapohitaji. Ikiwa unafanya kazi, omba ruhusa ya mapumziko kama itawezekana.

Hakikisha kuwa unakula chakula kilicho na afya na ufanye mazoezi. Ukifanya mambo hayo mawili utasaidika mno.

Kushiriki katika aina fulani ya mapumziko yaweza kuwa na msaada pia. Jihusishe na mambo ambayo unajua yatakupumzisha. Oga. Tembea. Sikiliza baadhi ya muziki utakaokuridhisha. Soma baadhi ya vitabu au magazeti ya kuchekesha /kufurahisha (manga)au tazama vipindi vya vibonzo/katuni.

Wakati wowote ule, fanya mambo ambayo hukufurahisha. Jiruhusu kuanza kufurahia maisha tena. Usijilaumu au kuhisi vibaya ukijipata ukitabasamu, kuwa na wakati mzuri au furahia maisha baada ya hasara yako. Haumsaliti mwenzako aliyeaga unapochukua hatua ya kupona.

Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020921