Mbona nishiriki ngono iliyo salama

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Mbona_nishiriki_ngono_iliyo_salama

Click Code to Download

Kama maambukizi mengine ambayo watu hupata, magonjwa ya zinaa husababishwa na viini. Maambukizi mengine husababishwa na viini vilivyo hewani, kwenye chakula au maji. Magonjwa ya zinaa husambazwa kwa njia ya ngono. Magonjwa mengine ya zinaa husababisha vidonda au kutokwa kwenye sehemu za uzazi, lakini huwezi kutambua ikiwa mtu anaugua ugonjwa wa zinaa kwa kumtazama tu. Baadhi ya wanawake na wanaume wanaweza kuwa na ugonjwa wa zinaa bila ya wao wenyewe kujua. Viini vinavyosababisha baadhi ya magonjwa ya zinaa kama vile vidonda kwenye sehemu za uzazi au malengelenge huwa kwenye ngozi ya sehemu hizi za uzazi na husambazwa kwa ngozi kugusana.

Viini vinavyosababisha magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, chlamydia, hepatitis na virusi vya HIV huishi kwenye umajimaji ulioko kwenye mwili wa mtu aliyeambukizwa. Husambazwa kupitia kwenye damu, shahawa, au umajimaji kwenye uuke wa mtu aliyeambukizwa - ukigusa ngozi ya uuke, sehemu ya kutoa haja kubwa au ncha ya uume, au mdomo wa mtu mwingine. Kushiriki ngono salama inamaanisha kuwa, kusiwe na kugusana kwa ngozi ya wapenzi wote wawili hasa kwa umajimaji, isipokuwa tu ukiwa na uhakika kuwa mpenzi wako hana ugonjwa wa zinaa. Maambukizi haya yote yanaweza kusababisha shida za kiafya. HIV ni hatari sana ikiwa utakosa kupata matibabu ya mara kwa mara.

Kushiriki ngono na wapenzi wengi, au isiyo salama, humweka mwanamke katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa zinaa, ikiwemo HIV. Hiv inaweza kusababisha kifo kutokana na UKIMWI. Magonjwa ya zinaa yasipotibiwa yanaweza kusababisha utasa, uja uzito kwenye mishipa, na mimba kuharibika. Kuwa na wapenzi wengi pia humweka mwanamke katika hatari ya kuugua pelvic infammatory disease na saratani. Wanawake na wanume wanaweza kusaidia kuzuia shida hizi zote kwa kushiriki ngono salama.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010508