Nafaa kujua nini kuhusu kushiriki ngono

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nafaa_kujua_nini_kuhusu_kushiriki_ngono

Click Code to Download

  • Unaweza kushika mimba mara ya kwanza ukishiriki ngono.
  • Unaweza kushika mimba wakati wowote unaposhiriki ngono bila kutumia mbinu yoyote ya kupanga uzazi (hata kama ni mara moja tu).
  • Unaweza kushika mimba hata ikiwa mwanaume anafaikiri kuwa hakumwaga mbegu zake.
  • Unaweza kuambukizwa ugonjwa wa zinaa au virusi vya HIV usipotumia kondomu unaposhiriki ngono na mtu aliyeambukizwa. Huwezi kujua ikiwa ameambukizwa kwa kumtazama tu.
  • Ni rahisi kwa msichana kuambukizwa magonjwa ya zinaa au virusi vya HIV kutoka kwa mvulana au mwanaume, ikilinganishwa na yeye kumuambukizamwanaume. Hii intokana na jinsi tendo la ngono hufanyika - kwa sababu yeye ndiye anayepokea. Pia, ni vigumu kujua ikiwa msichana ana maambukizi kwa sababu yako ndani ya mwili wake.

Tumia kondomu wakati wote ili ujikinge kutokana na magonjwa ya zinaa na virusi vya HIV. Njia hakika ya kuepuka kushika mimba, magonjwa ya zinaa na virusi vya HIV ni kutoshiriki ngono.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020811