Nawazaje kuwa na maisha mazuri ya usoni

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nawazaje_kuwa_na_maisha_mazuri_ya_usoni

Click Code to Download

Jaribu kupanga maisha yako ya usoni.

Kitu cha kwanza cha kufanya kupanga maisha yako ya usoni ni kuweka malengo. Lengo ni jambo amabalo ungependa litendeke.

Kwa wasichana wengi, hii si rahisi. Wengi husikia kama maisha yao yanapangwa na familia au tamaduni za jamii zao. Lakini unaweza kujisaidia kwa kujua unayotaka maishani.

Pili, jaribu kuongea na mwanamke au mwanamume anayefanya jambo unalotaka kufanya. Inaweza kuwa mtu unayetamani au kiongozi katika jamii yako. Ulizia ikiwa unaweza kupata muda wa kujifunza zaidi kuhusu kazi yake.

Wakati mwingine wasichana huvunjika moyo kwa sababu maono na imani yao ya siku za usoni inapingana na mila za kijamii kuhusu kazi mwanamke anafaa kufanya. Ni muhimu kuwaeleza wazazi wako maono yako kwa utaratibu na pia kusikiliza maoni yao.

Tafuta mtu unayeweza kuzungumza naye ambaye unajuwa atakusikiza na kukuelewa---rafiki, dadako au jamaa wa kike. Zungumziakuhusu uoga na shida. Kwa pamoja mnaweza kuzungumzia kuhusu wanawake waliofaulu katika eneo lenu, malengo na maono ya siku za usoni.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020805