Nawezaje kumlinda mtoto wangu kutokana na ajali zinazotokana na sumu

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nawezaje_kumlinda_mtoto_wangu_kutokana_na_ajali_zinazotokana_na_sumu

Click Code to Download

Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa unaweka sumu hizi mahali ambapo watoto hawatazifikia.

Usiweke sumu kwenye chupa za soda au pombe, vikombe au mitungi, kwa sababu watoto wanaweza kuzikunywa kwa bahati mbaya. Weka madawa yote, kemikali na sumu kwenye vyombo vyake maalum, zifunge sawasawa na uziweke mahali ambapo watoto hawawezi kuzifikia.

Usiache sabuni za kawaida, sabuni kali (bleach) na madawa mahali ambapoi watoto wanaweza kuzifikia. Hakikisha kuwa zimewekwa kwenye vyombo ambavyo vimefungwa na kuandikwa majina sawasawa. Hakikisha kuwa sumu hizi zimefungiwa kwenye kabati au kuwekwa juu kwenye rafu, ambapo watoto hawawezi kufikia.

Madawa ya watu wazima yanaweza kuua au kusababisha majeraha kwa watoto wadogo. Ni jambo la muhimu kumpatia mtoto dawa alizoagizwa na daktari. Usimpe mtoto dawa iliyoagizwa kwa mtu mzima au mtoto mwingine. Hakikisha kuwa mtoto hachukui dawa mwenyewe. Ni wajibu wa mzazi au mlezi kumpa mtoto huyo dawa wakati unaohitajika. Hakikisha kuwa madawa yote yanahifadhiwa mahali ambapo watoto hawawezi kuyafikia.

Unaweza kutumia kabati ambazo haziwezi kufunguliwa na watoto kwa urahisi, kwa kuhifadhi sumu.


Sources