Nawezaje kushiriki ngono iliyo salama

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nawezaje_kushiriki_ngono_iliyo_salama

Click Code to Download

Jikinge kutokana na HIV na magonjwa mengine ya zinaa: vaa kondomu kabla sehemu za uzazi za mpenzi wako hazijagusa zako.

Tendo la ngono huja na hatari zake, lakini kuna njia za kulifanya liwe salama. Tusema ngono "salama" kama njia ya kuwakumbusha watu kuwa hatari ndogo sio sawa na ukosefu wa hatari. Lakini, ngono iliyo "salama" inaweza kuokoa maisha yako.

Ni wajibu wa kila mwanamke kuamua ni kiwango kipi cha hatari atakikubali, na hatua hatua za kuhakikisha kuwa ngono ni salama. Hapa chini kuna njia ambazo wanawake wanaweza kutumia kupunguza hatari:

Salama kabisa:

 • Epuka kushiriki ngono kabisa. Ikiw ahutashiriki ngono, hautakuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Baadhi ya wanawake huona huu ni uamuzi bora, hasa wakiwa na umri mdogo. Lakini, kwa wanawake wengine uamuzi huu hauwezekani.
 • Shiriki ngono na mpenzi mmoja pekee, ambaye unajua kwa kweli anashiriki ngono na wewew tu, na unafahamu kuwa hakuna kati yenyu alikuwa ameambukizwa ugonjwa wa zinaa hapo mbeleni. Hii inaweza kujilikana tu kwa kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya zinaa.
 • Mnaweza kushiriki ngono kwa kupapasana sehemu za uzazi.
 • Tumieni kondomu wakati mnashiriki ngono (ikiwa mtatumia midomoyenyu). Kondomu husaidia kuzuia maambukizi kama vile malengelenge na kisonono kwenye koo. Pia hukulinda kutokana na hatari ndogo ya kuambukizwa virusi vya HIV kupitia mipasuko midogo mdomoni.

Salama:

 • Tumia kondomu wakati wote - ya wanaume au ya wanawake - unaposhiriki ngono ya aina yoyote.
 • Mnaposhiriki ngono, hakikisha kuwa majimaji kutoka kwa sehemu yako ya uzazi haimuingii mwenzako kwenye sehemu ya uzazi au njia ya haja kubwa. Sio rahisi kusambaza virusi vya HIV kwa kushiriki ngono aina ya mdomoni. Ukiingiwa na shahawa mdomoni, iteme mara moja.

Hatari kidogo:

 • Hakikisha kuwa mwanaume ametoa uume wake ndani yako kabla hajamwaga shahawa. Unaweza kuambukizwa virusi vya HIV au kushika mimba, lakini hakuna uwezekano mkubwa kwani ni shahawa kidogo sana itaweza kuingia mwilini mwako.
 • Utumizi wa mbinu aina diaghragm ya upangaji uzazi inaweza kupunguza hatari.
 • Epuka kushiriki ngono ikiwa sehemu yako ya uzazi imekauka kwani hukwaruzika kwa urahisi, na kuongeza uwezekano wa kupata maambukizi. Tumia mate, ili kufanya sehemu yako ya uzazi kuteleza. Usitumie mafuta ya kupika au mafuta yenye marashi ikiwa unatumia kondomu - kwani yanaweza kuifanya kondomu ipasuke.
 • Ikiwa una ugonjwa wowote wa zinaa, pata matibabu. Uwepo wa ugonjwa mmoja wa zinaa hurahisisha maambukizi kutokana na HIV au magonjwa mengine ya zinaa.
Sources
 • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
 • Audiopedia ID: sw010510