Nawezaje kuzuia kupata mimba kwa kunyonyesha katika miezi 6 ya kwanza

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nawezaje_kuzuia_kupata_mimba_kwa_kunyonyesha_katika_miezi_6_ya_kwanza

Click Code to Download

Kunyonyesha kunaweza kuzuia mwili kutengeneza yai. Mbinu hii haina gharama yoyote, lakini inaweza kutumika tu katika miezi 6 baada ya kujifungua pekee.

Kunyonyesha ni mbinu mwafaka ya kupanga uzazi, lakini sharti mambo yafuatayo yazingatiwe:

1. Mtoto wako yuko na umri wa chini ya miezi 6.

2. Haujapata hedhi tangu kujifungua.

3. Unamnyonyesha tu mtoto wako, na hii ni kila mara anapohisi njaa, usiku na mchana, na haupitishi masaa 6 kabla hujamnyonyesha. Mtoto wako halali usiku kucha bila kunyonya.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020503