Nawezaje kuzuia magonjwa ya zinaa

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nawezaje_kuzuia_magonjwa_ya_zinaa

Click Code to Download

Kuzuia magonjwa ya zinaa kunaweza kukulinda wewe na mpenzi wako kutokana na magonjwa hatari na utasa.

Shiriki ngono salama.

Tumia kondomu kila unaposhiriki ngono. Kondomu za kike na za kiume:

  • zitakulinda kutokana na magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV.
  • zitalinda afya ya mpenzi wako.
  • zitazuia mimba ambazo hazijapangiwa. Tumia mojwapo ya kondomu hizi unaposhiriki ngono - na wala sio zote mbili kwa pamoja.

Ikiwa mpenzi wako hatatumia kondomu, diaghragm itakulinda kutokana na magonjwa fulani ya zinaa, hasa kisonono na chlamydia.

Osha nje ya uuke wako baada ya kushiriki ngono.

Nenda haja ndogo baada ya kushiriki ngono.

Usitumie miti shamba au poda kukausha uuke wako. Unaotumia maji na sabuni kuosha ndani ya sehemu yako ya uzazi, unaleta hitilafu na namna asilia ya uke wako ambayo huiweka ikiwa na afya. Sehemu yako ya uzazi ikikauka, unaweza kuhisi uchungu wakati wa ngono. Hii hukuweka katika hatar ya kuambukizwa virusi vya HIV na magonjwa mengine ya zinaa.

Wewe na mpenzi wako mnaweza kushiriki aina zingine za kuonyeshana mapenzi badala ya kushiriki ngono.

Msishiriki ngono, ikiwa wewe na mpenzi wako mna ishara za ugonjwa wa zinaa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010509