Nawezaje kuzungumza na mpenzi wangu kuhusu ngono salama

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nawezaje_kuzungumza_na_mpenzi_wangu_kuhusu_ngono_salama

Click Code to Download

Ukiona kuwa mpenzi wako anakuunga mkono katika uamuzi wako wa kushiriki ngono salama, jaribu kuzungumza naye kuhusu madhara ya magonjwa ya zinaa kwa afya. Jambo hili sio rahisi! Wanawake wengi hufundishwa kuwa sio vizuri kuzungumzia mambo ya ngono - hasa na wapenzi wao au wanaume wengine - hivyo basi hawana uzoefu. Mwanaume anaweza kuzungumza na wanaume wengine kuhusu ngono, lakini huona aibu kuzungumza na mpenzi wake. Hapa kuna mapendekezo:

  • Angazia usalama. Unapozungumzia ngono salama, mpenzi wako anaweza kusema kuwa wewe huna imani naye. Lakini jambo la muhimu ni usalama, wala sio imani. Kwa vile huenda mtu anaugua ugonjwa wa zinaa bila kujua, au aliambukizwa virusi vya HIV kwa njia nyingine, ni vigumu sana kwa mtu kuwa na uhakika kuwa hajaambukizwa. Ngono salama ni wazo nzuri kwa wapendanao, hata kama wapenzi hawa hushiriki ngono kati yao pekee.
  • Fanya mazoezi kwa kuzungumza na rafiki yako kwanza. Muulize rafiki yako ajifanye kuwa mpenzi wako, kisha fanya mazoezi ya yale ungependa kumwambia. Jaribu kufikiria kuhusu baadhi ya mambo ambayo atakubaliana nayo. Kumbuka kuwa huenda ataona hayakuzungumza, kwa hivyo jaribu sana kumpa hakikisho.
  • Usisubiri hadi wakati mnataka kushiriki ngono ndio uanze kuzungumzia mambo haya. Chagua wkati ambapo nyote mna furaha. Ikiwa mmeacha kushiriki ngono kwa sababu mna mtoto mchanga, au mlikuwa mnatibiwa ugonjwa wa zinaa, jaribuni kuzungumza kabla ya kushiriki ngono tena. Ikiwa wewe na mpenzi wako mnaishi mbali mbali, au kila wakati lazima msafiri, zungumzeni mapema jinsi ya kulinda afya yenyu ya kingono.
  • Jifunze mengi kuhusu athari za ngono isiyo salama, na jinsi ya kushiriki ngono salama. Ikiwa mpenzi wako hafahamu mengi kuhusu magonjwa ya zinaa, jinsi yanavyosambazwa, na madhara yake, huenda hataelewa athari zinzohusiana na ngono isiyo salama. Ni muhimu apate habari itakayomuezesha kufahamu umuhimu wa ngono salama.
  • Tumia watu wengine kama mfano. (Ndugu yangu aliniambia kuwa yeye hutumuia kondomu kila mara). Ni vyema mpenzi wako akifahamu kuwa watu wengine wanashiriki ngono salama. Hii itampa motisha kufanya hivyo pia.Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010511