Ni aina gani za ukatili dhidi ya wanawake bado zipo

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Ni_aina_gani_za_ukatili_dhidi_ya_wanawake_bado_zipo

Click Code to Download

Kuna njia nyingi tofauti ambazo mwanamume hujaribu kutumia kupata mamlaka kwa mwanamke. Kumpiga ni mmoja yazo. Lakini njia hizo zote zinaweza kumuumiza mwanamke:

Unyanyasaji wa kihisia: Mwanamume humtusi mwanamke, humdhalilisha, au humfanya afikirie ni mwendawazimu.

Kudhibiti Pesa/Fedha: Mwanamume hujaribu kumfanya mwanamke akose kupata kazi au kutengeneza pesa zake mwenyewe. Humfanya amuitishe pesa zozote anazohitaji. Au anaweza kumlazimisha kufanya kazi, kisha achukue mapato yake.

Unyanyasaji wa kijinsia: Mwanamume humfanya mwanamke kufanya mambo ya kingono bila hiari ya mwanamke, au kumshambulia kingono katika sehemu zake za mwili. Humbeba kama kifaa.

Kumlaumu: Mwanamume husema kwamba dhuluma haikutendeka, kwamba haikuwa mbaya hivyo, au kwamba ilikuwa kosa la mwanamke.

Kwa kutumia watoto: Mwanamume hutumia watoto kumfanya mwanamke kuhukumika, au kumdhuru.

Kwa sababu Yeye Ni 'Mwanaume': Mwanamume hutumia ukweli kwamba yeye ni mwanamume kama kisingizio cha kumfanya mwanamke awe mtumishi. Hufanya maamuzi yote na kumwambia kuwa, kama mwanamke, hana haki ya kupinga.

Vitisho: Mwanamume hutumia umbo lake, hatua, sauti, au hufanya vitisho vinavyo mfanya mwanamke kuhisi hofu na kuogopa kuumizwa.

Kutengwa: Mwanamume hudhibiti kila kitu mwanamke afanyacho- anayemuangalia, anayezungumza naye na anakoenda

Aina moja ya dhuluma husababisha aina nyingine ya dhuluma. Mamlaka na utawala ni mambo yanayosababisha hayo yote.

Katika visa vingi, matusi husababisha unyanyasaji wa kimwili baada ya muda. Haiwezi kuonyesha hapo mwanzo, lakini polepole mwanamume huanza 'kwa bahati mbaya' kumsukuma au kumgonga mwanamke, au huanza kukaa katika sehemu ya mwanamke ndiposa mwanamke alazimike kuhama sehemu nyingine. Ikiwa tabia hii itafaulu, inaweza kuwa mbaya hadi aanze vurugu. Si wanawake wote ambao hunyanyaswa kupitia aina zingine, huchapwa, lakini wanawake wote waliochapwa wameteseka kutokana na aina nyingine za unyanyasaji.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020106