Nifanyeje ikiwa nina ishara za ugonjwa wa zinaa au niko hatarini ya ugonjwa wa zinaa

Kutoka Audiopedia Swahili
Rukia: urambazaji, tafuta
QR for this page

https://www.audiopedia.org/sw/Nifanyeje_ikiwa_nina_ishara_za_ugonjwa_wa_zinaa_au_niko_hatarini_ya_ugonjwa_wa_zinaa

Click Code to Download

Ikiwa una ishara ya ugonjwa wa zinaa, au unafikiri kuwa uko katika hatari ya ugonjwa wa zinaa, lazima utafute matibabu mara moja. Kwa bahati mbaya, uchunguzi wa magonjwa ya zinaa hayapatikani katika sehemu nyingi, labda kwa sababu ni ghali na wakati mwingine hautoi matokeo kamili. Ukosefu wa huduma za bei nafuu, zinazotoa matokeo kamili kwa uchunguzi wa magonjwa ya zinaa ni shida kubwa sana kwa wanawake. Husababisha wanawake kumeza dawa ambazo hawahitaji, hawawezi kuzigharamia na ambazo zina madhara.

  • Tibu maambukizi mara moja.
  • Usingoje hadi uwe mgonjwa sana. Matibabu yatasaidia kukulinda kutokana na shida zingine baadaye, na zitasaidia kuzuia kusambazwa kwa magonjwa ya zinaa kwa watu wengine.
  • Hakikisha kuwa unapimwa, ikiwa kuna huduma za kupimwa. Unaweza kuwa umeambukizwa na ugonjwa wa zinaa na ukose kuwa na ishara.
  • Hakikisha kuwa mpenzi wako pia anapata matibabu kwa wakati. Ikiwa hatapata matibabu, atakuambukiza mtakaposhiriki ngono.
  • Hakikisha mnashiriki ngono salama. Unaweza kuambukizwa ugonjwa mwingine wa zinaa au virusi vya HIV ikiwa hautajikinga.
  • Nenda ukapimwe virusi vya HIV. Magonjwa ya zinaa na virusi vya HIV huambatana.
  • Nunua na umeze dawa zote ambazo umepatiwa. Hata ishara zikitokomea, hautakuwa umepona hadi pale ambapo madwa yatakuwa yamefanya kazi. Ikiwa ishara hazitokomei baada ya kumeza dawa, muone mhudumu wa afya. Uchungu au kutokwa kwenye uuke husababishwa na saratani.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010507